Subscribe Us

Breaking News

Jeshi la polisi Tanzania lapiga marufuku maandamano ya Desemba 9, 2025


.

Chanzo cha picha,Jeshi la polisi

Msemaji wa Polisi David Misime, amepiga marufuku kufanyika kwa maandamano ya Desemba 9, 2025, ambayo yamepangwa kufanyika nchi nzima.

"Maandamano hayo yamekosa sifa za kisheria za kuyaruhusu kufanyika…na kwamba upo uhalifu unaoendelea kupangwa na kuhamasishwa kwenye mitandao ya kijamii na kwenye makundi ya baadhi ya watu wakihamasisha kile wanachokiita maandamano ya amani na yasio na kikomo…," amesema msemaji wa polisi.

Msemaji wa polisi ameweka wazi kuwa bado hakuna barua waliopokea inayotoa taarifa ya kufanyika kwa maandamano hayo.

Jeshi la polisi limetoa wito kwa wananchi na wale wasio raia wa Tanzania waliopo ndani yan chi hiyo kuepuka maandamano hayo.


 

Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments