Subscribe Us

Breaking News

Meta yajibu sababu za kufungia akaunti za wanaharakati wawili wa Tanzania

h

Chanzo cha picha,Mange Kimambi/Instagram

Kampuni ya Meta imesimamisha akaunti za Instagram za wanaharakati wawili wa Tanzania baada ya kuchapisha picha na video zinazoonesha jinsi watu walivyoumizwa au kuuawa na maafisa wa usalama wa Tanzania wakati wa vurugu zilizozuka wakati wa uchaguzi wa Oktoba 29.

Kulingana na mashirika ya kutetea haki za binadamu na upinzani, zaidi ya watu elfu moja waliuawa katika ghasia hizo lakini mpaka sasa Serikali ya Tanzania haijatoa takwimu zozote kuhusu idadi ya waliojeruhiwa au kuuawa wakati wa uchaguzi ambao waangalizi wa kimataifa waliutaja kutokuwa huru wala wa haki.

Mange Kimambi ambaye ana zaidi ya watu milioni mbili na laki tano wanaomfuatilia Instagram amefutiwa akaunti yake ya Instagram na Whatsapp na kampuni ya Meta.

Mwanaharakati mwingine anayeishi uhamishoni Maria Sarungi pia akaunti yake ya Instagram haiwezi kuonekana Tanzania.

Msemaji wa Meta aliieleza BBC kwamba akaunti zake za Instagram, akirejelea Mange Kimambi, “zimeondolewa kwa kukiuka sera yetu ya kukiuka masharti mara kwa mara.”

Msemaji wa serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa, aliambia BBC kwamba anapaswa “kutoa uthibitisho wa madai yake.”

“Hatukubali watu kufungua akaunti mpya zinazofanana na zile tulizowahi kuondoa kwa kukiuka Viwango vyetu vya Jumuiya,” alisema.

Jumatatu, Samia alisema kuwa serikali yake iko tayari kukabiliana na waandamanaji katika maandamano mapya yaliyopangwa kufanyika Jumanne ijayo.

Kimambi alibainisha kuwa siku hiyo hiyo akaunti zake zilipofutwa, zile za mwanaharakati mwingine maarufu wa Tanzania, Maria Sarungi, zilizuiwa.

“Ninaamini hili linatoa ushahidi zaidi kwamba Meta inaweza kuwa ilishinikizwa na serikali ya Tanzania kunyamazisha sauti zinazozungumza kwa niaba ya wananchi,” aliandika katika ukurasa wake wa X, ambao bado unapatikana.

Pia alimuomba Rais wa Marekani, Donald Trump, kuishinikiza Meta kurejesha kurasa zake.

“Kwa miezi kadhaa, nimetumia majukwaa yangu kuangazia masuala haya na mara kwa mara kuhimiza 'maandamano ya amani', kwani Watanzania wengi wanahisi hakuna njia salama ya kuonyesha kutoridhika kwao,” alisema.

Kuondolewa kwa akaunti za Kimambi kunakuja wakati ambapo Marekani imesema inakagua upya uhusiano wake na Tanzania, ikitaja kuongezeka kwa wasiwasi kuhusu kuporomoka kwa misingi ya demokrasia na ukiukaji wa haki za binadamu.

Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Washington imeishutumu serikali ya Tanzania kwa kukandamiza uhuru wa kidini na uhuru wa kujieleza, kuzuia uwekezaji wa Marekani, na kushindwa kuzuia machafuko kabla na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29.

Imesema hatua hizo zimeweka raia wa Marekani, watalii na maslahi ya Marekani hatarini, na zinatishia miongo kadhaa ya ushirikiano katika usalama na maendeleo.

“Mustakabali wa uhusiano wetu wa pande mbili utategemea hatua za serikali,” taarifa hiyo imesema.

Mamlaka za Tanzania bado hazijajibu.

Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore kwa sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments