Subscribe Us

Breaking News

Dereva afariki ajali ya gari la mizigo Babati

 

Dereva wa gari la mizigo aina ya Scania Semi Lenye namba za usajili T739 EDV,Maulidi Juma mkazi wa Arusha anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 32, amefariki dunia katika ajali iliyotokea eneo la Sigino, barabara ya Singida–Babati, baada ya gari hilo kufeli breki na kupinduka.

Ajali hiyo imetokea Februari 5, majira ya saa mbili Usiku, katika kata ya Sigino, wilaya ya Babati, mkoani Manyara na Kwa mujibu wa mashuhuda, gari hilo lilipata hitilafu ya breki na kupinduka wakati dereva huyo akijaribu kumkwepa mwendesha bodaboda.

Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika katika eneo la tukio na kufanya jitihada za kuokoa mwili wa dereva huyo. Baada ya juhudi hizo, mwili wake umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa ajili ya taratibu zaidi.

Tukio hilo limeacha simanzi miongoni mwa wakazi wa eneo hilo, huku Mwenyekiti wa Wa kitomgoji Cha Sigino akitoa tahadhari kwa watumiaji Barabara kuwa waangalifu kwani eneo Hilo linasifika kwa ajali nyingi.

No comments