Kocha wa Fountain Gate atangaza kuwa shabiki lialia wa Simba

Katika jambo lisilokuwa la kawaida ndani ya mpira wa Tanzania Bara Kocha wa klabu ya Fountain Gate ambaye ni Raia wa Kenya Robert Matano ameweka wazi kuwa yeye ni Shabiki lialia wa klabu ya Simba kwa miaka Mungu na hata jina lake jingine anajiita Simba.

Ikumbukwe leo 6/2/2025 ni siku ya mchezo kati ya Fountain Gate dhidi ya Simba utakaopigwa katika Dimba la Tanzanite Kwaraa Stadium Manyara majira ya Saa 10:15 jioni.

Kauli hii imeibua maneno mengi sana mitandaoni hususani kwa wadau wa Soka.
Je wewe kama mdau wa Soka la Tanzania Bara unaichukuliaje kauli hii ikiwa mchezo wenyewe unachezwa leo hii??
Na iwapo Fountain Gate atafungwa na Simba hii kauli ya Kocha wao haitokuwa na mashaka kweli??



No comments