Subscribe Us

Breaking News

Mgogoro wa kisheria unanukia huku Trump akijaribu kikomo cha mamlaka ya urais

 


.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Rais Donald Trump

Katika wiki za kwanza za muhula wake wa pili, Rais Donald Trump hajapoteza muda katika kuonyesha misuli yake ya kisiasa. Hiyo ni wazi kabisa.

Tangu aingie madarakani mwezi Januari, ameamuru kusimamishwa kwa madai yote mapya ya watu wanaotafuta hifadhi, kughairi makazi mapya ya wakimbizi, uajiri na matumizi ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali yaliyoanzishwa na Congress.

Kimbunga cha hatua zake kutoka kwa ahadi zake za kampeni kimevuka mipaka ya mamlaka ya urais - na kusababisha changamoto za kisheria kutoka kwa Wanademokrat, vyama vya wafanyakazi na makundi ya kisheria.

Kufikia sasa mahakama za majimbo zimekuwa vizuizi vya ajenda ya Trump, kwani majaji wamesimamisha kwa muda baadhi ya mapendekezo yenye utata, ikiwa ni pamoja na kukomesha uraia wa moja kwa moja kwa mtu yeyote aliyezaliwa katika ardhi ya Marekani.

Lakini Trump anaendelea - na anaonekana kuelekea kwenye mzozo ambao hatimaye unaweza kuishia katika mahakama ya juu zaidi nchini.

Wiki hii, jaji wa Rhode Island alisema utawala wa Trump ulikuwa umekaidi waziwazi agizo lake la mahakama la kufungia mabilioni ya fedha za majimbo. Ikulu ya White House ilijibu kwa kusema kwamba "kila hatua" ambayo rais alichukua ilikuwa "halali kabisa".

No comments