Subscribe Us

Breaking News

Vita vya Ukraine: Putin 'hayuko tayari kwa mazungumzo ya amani'- Zelensky

 


gg

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Rais wa Ukraine Volodimir Zelensky amejibu shambulizi lililofanyika mapema Jumatano limeonesha kuwa Rais Putin wa Urusi “hayuko tayari kwa mazungumzo ya amani” na anaendelea na mashambulizi dhidi ya raia wa Ukraine na kuharibu miji.

Haya yanajiri baada ya shambulizi lililotekelezwa na Urusi dhidi ya Ukraine mapema Jumatano limeacha watu wawili wakiwa wameuawa na wanne wakijeruhiwa, akiwemo msichana wa miaka 9, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa meya wa Kyiv, Vitali Klitschko.

Wanajeshi wa Ukraine walithibitisha kwamba walidungua vilipuzi sita kati ya saba pamoja na ndege zisizo na rubani 71 zilizotumika katika shambulizi hilo.

Shambulizi hilo lililenga maeneo mbalimbali katika viunga vya Kyiv, ikiwemo Holosiivskyi, Podilskyi, Sviatoshynskyi, na Obolonskyi.

Hali hii inatokea wakati ambapo Rais Volodymyr Zelensky ametangaza kuwa Ukraine iko tayari kubadilishana ardhi na Urusi ikiwa wataingia mazungumzo ya amani.

Aidha, Zelensky anatarajiwa kukutana na Makamu wa Rais wa Marekani, Jd Vance, ambaye amekuwa akikosoa msaada wa kijeshi kutoka Marekani kwa Ukraine.

Hata hivyo, serikali ya Marekani imetangaza kuwa iwapo itaendelea kusaidia Ukraine kupigana na Urusi watahitaji kupatiwa rasilimali ghafi zilizoko nchini humo.

No comments