Subscribe Us

Breaking News

Mtoto wa Bashar al-Assad azungumza kwa mara ya kwanza tangu kuanguka utawala wa baba yake

 


F

CHANZO CHA PICHA,SOCIAL MEDIA

Maelezo ya picha,Hafez al-Assad

Mtoto wa Rais wa zamani wa Syria, Bashar al-Assad, aitwaye Hafez ameonekana kwenye kipande cha video kwa mara ya kwanza tangu babake kuondolewa madarakani Desemba mwaka jana.

Katika video hiyo, ambayo ilitolewa Februari 12, Hafez al-Assad anaonekana akitembea kwenye barabara ya juu ya Moscow wakati wa mchana.

Katika video hiyo, ambayo haizidi sekunde tisa, anathibitisha tu kwamba ana akaunti mbili ya Telegraph na X, akizungumza kwa lahaja ya Syria:

"Kuna na swali kuhusu ikiwa akaunti kwenye X na Telegraph ni zangu, kwa hivyo nataka kufafanua: Ndio, ni zangu na sina akaunti nyingine kwenye jukwaa lolote.”

Hilo linakuja baada ya akaunti ya Telegram inayohusishwa na Hafez kupata umaarufu, akitoa maelezo ya saa za mwisho za utawala wa baba yake.

Hafez hataji kwa uwazi jina la akaunti yake ya Telegram kwenye video, lakini maneneo yaliyofifia yanaonekana yakionyesha akaunti hiyo hiyo iliyopata umaarufu chini ya jina lake.

BBC imechunguza video hiyo na kubaini ilirekodiwa kwenye Mtaa wa Bolshaya Ordynka katikati mwa Moscow, kama kilomita moja tu kutoka Ikulu ya rais ya Kremlin.

Haikuwezekana kuthibitisha ikiwa video hiyo ilirekodiwa siku ambayo ilichapishwa, Februari 12. Baadhi ya akaunti za mtandaoni zimeibua maswali kuhusu uhalisi wa video hiyo inayoambatana na uwezekano kwamba ilitolewa na akili bandia.

Maswali haya yalitokana na kuchelewa kidogo kati ya midomo ya Hafez al-Assad na sauti yake. Hata hivyo, ucheleweshaji huu unaweza kutokana na sababu mbalimbali kama vile jinsi video inavyopakiwa au matatizo ya kiufundi wakati wa kurekodi.

Hakuna dalili dhahiri katika video hiyo zinazoonyesha kuwa ilitolewa na akili bandia. Teknolojia mbili za utambuzi wa uso zilizotumiwa na BBC zilimtambua mtu huyo kwenye video kuwa ni Hafez al-Assad, kwa uhakika wa karibu asilimia 100.

No comments