Mzozo wa DRC: Miili ya wanajeshi wa Afrika Kusini waliouawa katika mapigano yarejea nyumbani

Miili ya wanajeshi 14 wa Afrika Kusini waliouawa mashariki mwa DRC mwezi uliopita yamerejeshwa nchini humo baada ya kucheleweshwa kwa muda mrefu.
Wanajeshi hao walipoteza maisha walipokuwa wakipigana na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda katika mjini Goma.

Takriban wanajeshi 800 waliripotiwa kupelekwa katika eneo hilo mapema wiki hii lakini SANDF imekataa kuthibitisha taarifa hizo . Jeshi la Afrika Kusini (South African National Defence Union) limesema kuwa suala hilo lilikuwa nyeti kwasababu taarifa yoyote itahatarisha maisha ya askari wa ardhini.
Ibada ya kuwakumbuka wanajeshi waliofaliki imefanyika katika kambi ya jeshi la anga la Swartkop mjini Johannesburg.
No comments