Subscribe Us

Breaking News

RSF yauwa mamia ya raia ndani ya siku chache zilizopita Sudan

 Picha ya wapiganaji wa RSF Sudan

Picha ya wapiganaji wa RSF Sudan

Mashambulizi kutoka kwa kundi la kijeshi la Rapid Support Forces la Sudan yameua mamia ya raia wakiwemo watoto, kwenye jimbo la White Nile, maafisa wa serikali na makundi ya haki za binadamu wamesema Jumanne.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Sudan kupitia taarifa imesema kuwa RSF ililenga raia ndani ya siku kadhaa zilizopita kwenye vijiji vilivyopo eneo la al-Gataina baada ya kushindwa vikali na jeshi la serikali.

Taarifa hiyo imeweka idadi ya vifo kuwa 433, wakati Kamati ya Madaktari wa Sudan ikiorodhesha idadi ya 300. Mawakili wa dharura ambao wameunda kundi la haki za binadamu linalofuatilia ghasia dhidi ya raia, kupitia taarifa ya Jumanne wamesema kuwa zaidi ya watu 200 wakiwemo wanawake na watoto waliuwawa kwenye mashambulizi ya RSF, huku mamia wengine wakijeruhiwa ndani ya siku 3 zilizopita.

Mashambulizi hayo yanajumuisha mauaji, utekaji nyara, kupotezwa kwa nguvu, wizi na kupigwa risasi kwa wale waliyokuwa wakijaribu kutoroka taarifa zimeongeza. Waziri wa Utamaduni na Taarifa, Khalid Ali Aleisir, kupitia Facebook alisema kuwa mashambulizi ya RSF kwenye vijiji vya Al-Kadaris na Al-Khalwat katika jimbo la White Nile, yakiwa mahambulizi ya karibuni zaidi dhidi ya raia wasio na ulinzi.

No comments