Subscribe Us

Breaking News

Tetesi za Soka Ulaya: Villa yamtaka Rashford kwa uhamisho wa kudumu

 


Marcus Rashford

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Marcus Rashford

Mshambuliaji wa Manchester United na England, Marcus Rashford, 27, yuko tayari kubadilisha uhamisho wake wa mkopo wa Januari kwenda Aston Villa kuwa wa kudumu. (Sun)

Barcelona na Bayern Munich pia zinamfuatilia Rashford kwa karibu. (Football Insider)

Liverpool wanaonesha nia kubwa ya kumnasa mshambuliaji wa Newcastle na Sweden, Alexander Isak, huku Arsenal pia wakimmendea kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Times)

Arsenal huenda wakalazimika kumuuza mshambuliaji wao Mbelgiji, Leandro Trossard, 30, au winga wao Mbrazil, Gabriel Martinelli, 23, ili kufanikisha mchakato wa kuimarisha kikosi chao msimu ujao, huku wote wawili wakivifikiria vilabu vya ligi kuu ya Saudi Arabia. (Mirror)

 Leandro Trossard,

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Leandro Trossard

Victor Osimhen anatamani kuhamia Manchester United, ingawa klabu hiyo italazimika kushindana na timu kadhaa kubwa kumnasa mshambuliaji huyo wa Nigeria mwenye umri wa miaka 26, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Galatasaray akitokea Napoli. (Teamtalk)

Manchester United wako tayari kumuuza mshambuliaji wao wa Denmark, Rasmus Hojlund, 22, ili kumpata Osimhen. (Calciomercato)

Chelsea bado wana nia ya kumsajili winga wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Karim Adeyemi, ambaye thamani yake ni euro milioni 45 (£37.1m). (CaughtOffside)

Manchester City wanataka kumsajili kipa mpya kuchukua nafasi ya mlinda mlango wao wa Brazil, Ederson, 31, msimu huu wa joto, na klabu hiyo ipo kwenye mazungumzo na Porto kuhusu kipa wa kimataifa wa Ureno, Diogo Costa, 25.

Diogo Costa

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Diogo Costa

Bayern Munich wameondoa ofa yao ya mkataba mpya kwa kiungo wa Ujerumani, Joshua Kimmich, baada ya kuchoshwa na kusita kwake kusaini mkataba mpya. (Bild)

Barcelona wameonyesha nia ya kumsajili winga wa AC Milan, Rafael Leao, 25, kutoka Ureno. (Nicolo Schira)

Newcastle United wanataka kumsajili kipa wa Burnley, James Trafford, 22, kutoka England. (Football Insider)

Ligi Kuu ya England huenda ikalazimika kuwa na madirisha mawili tofauti ya usajili msimu huu wa joto kutokana na uwepo wa Kombe la Dunia la Vilabu. (Guardian)

No comments