Ujumbe wa Hamas wawasili Cairo kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano

Ujumbe wa Hamas umewasili Cairo kwa mazungumzo ya kusitisha mapigano, kwa mujibu wa vyombo vya habari vinavyoendeshwa na Hamas Filastin.
Kundi hilo limeanza mikutano na maafisa wa Misri kujadili utekelezaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Misri imekuwa mmoja wa wapatanishi wakuu katika mazungumzo kati ya Israel na Hamas.
Hapo awali, Hamas ilitoa taarifa ikisema inazishukuru Jordan na Misri kwa kukataa kuhama kwa Wapalestina.
Hii ilikuwa ni kujibu mpango wa Trump wa kuwahamisha Wapalestina kutoka Gaza na kuwapeleka katika mataifa mengine.
Wakati huo huo, Mustafa Barghouti, katibu mkuu wa mkakati wa kitaifa wa Palestina amesema kwamba matakwa ya Israel ya kutaka mateka wote waliozuiliwa na Hamas waachiliwe huru kufikia Jumamosi haiwezekani.
Huku mazungumzo ya amani yakianza kutokota shughuli za kawaida zimerejea Khan Younis eneo ambalo limekuwa likikumbwa na vita vya mara kwa mara.
Licha ya mchakato wa kusitisha mapigano Gaza kuendelea kutekelezwa, Israel bado inalenga mji wa Hezbollah ulioko Lebanon.
Hii ni baada ya Israel kuomba muda kabla ya kuondoa vikosi vyake kusini mwa Lebanon unaotarajiwa kukamilika Jumanne ijayo.
Israel sasa inataka wanajeshi wake wabaki katika sehemu tano nchini humo kwa siku zingine kumi, chanzo cha kidiplomasia ya Magharibi chaiambia BBC.
Serikali ya Lebanon inaendelea kujitahidi kurejesha uhuru wa nchi yao na mamlaka hiyo imepinga vikali kuchelewa kuondoka kwa wanajeshi wa Israel.
Kwa upande wa Israel imeapa kuendelea kushambulia kikosi kilicho n asilaha kinachoungwa mkono n aIran wakidai ni njia ya kukisambaratisha kisiendeleze na


No comments