Subscribe Us

Breaking News

YANGA 4-0 KEN GOLD, UWANJA WA KMC

 DAKIKA 45 mbele ya Ken Gold, Yanga inaongoza kwa mabao 4-0 ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa wababe hawa kukutana ndani ya msimu wa 2024/25.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Prince Dube dakika ya 2 na bao la pili likifungwa na Clement Mzize dakika ya 6 akapachika bao la nne dakika ya 42 dakika ya 38 Pacome alipachika bao la tatu kwenye mchezo.

Pacome anafikisha mabao 7 ndani ya ligi akiwa ni miongoni mwa viungo wenye mabao mengi kwa msimu wa 2024/25 akiwa sawa na Jean Ahoua wa Simba.

Mzize anafikisha mabao 9 akiwa ni namba moja kwa utupiaji ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar alifunga bao moja ikiwa ni mchezo wa mwisho kwa Sead Ramovic ambaye kwa sasa hayupo ndani ya Yanga.

No comments