China yawanyonga raia 4 wa Canada kwa uhalifu wa dawa za kulevya - Ottawa

Raia wanne wa Canada walinyongwa nchini China kwa mashtaka yanayohusiana na dawa za kulevya mapema mwaka huu, mamlaka ya Canada imethibitisha.
Wote walikuwa na uraia wa nchi mbili, na utambulisho wao umefichwa kwa ombi la familia zao, waziri wa mambo ya nje wa Canada Mélanie Joly aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.
Alilaani mauaji hayo kama "yasiyoweza kutenduliwa na hayaendani na utu wa msingi wa binadamu", akiongeza kuwa "aliomba binafsi msamaha".
Msemaji wa ubalozi wa China nchini Canada alisema ushahidi wa uhalifu wa raia hao wa Canada ulikuwa "dhabiti na wa kutosha" na kuitaka Canada "ikome kutoa matamshi ya kutowajibika", kulingana na ripoti.
Ubalozi wa China pia umeongeza kuwa Beijing "imehakikisha kikamilifu haki na maslahi ya raia wa Canada wanaohusika" na kuitaka serikali ya Canada kuheshimu "uhuru wa mahakama ya China".
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii



No comments