Subscribe Us

Breaking News

Mashambulizi ya Marekani yaua 53 huko Yemen

Idadi ya vifo kutokana na mashambulizi ya Marekani dhidi ya Yemen imeongezeka hadi 53, wakiwemo watoto watano, wizara ya afya ya waasi wa Houthi ilisema. Marekani ilisema ilianzisha mashambulio ya anga iliyoyaita “maamuzi yenye nguvu” katika maeneo yanayolengwa na Wahouthi siku ya Jumamosi, huku Rais Donald Trump akitaja sababu ya mashambulizi hayo ni kitendo cha Houthi kushambulia meli katika Bahari Nyekundu.

Washington ilisema baadhi ya watu muhimu wa Houthi walikuwa miongoni mwa waliofariki, lakini kundi hilo halijathibitisha hilo. Kiongozi wa Houthi Abdul Malik al-Houthi alisema kuwa wanamgambo wake watazishambulia meli za Marekani katika Bahari Nyekundu.

Akieleza ongezeko la idadi ya waliofariki hapo awali, msemaji wa wizara ya afya ya Houthi Anis al-Asbahi alichapisha kwenye X kwamba watu 53 wameuawa wakiwemo “watoto watano na wanawake wawili”, na kwamba watu 98 wamejeruhiwa.

Baba mmoja wa watoto wawili, aliyejitambulisha kwa jina la Ahmed, aliliambia shirika la habari la AFP: “Nimekuwa nikiishi Sanaa kwa miaka 10, nikisikia milio ya risasi katika muda wote wa vita. Wallahi sijawahi kukumbana na jambo kama hili hapo awali.”

Wahouthi pia walisema kulikuwa na mashambulizi mapya ya Marekani yaliyolenga Al Jaouf na Hudaydah mapema Jumatatu. Marekani bado haijatoa maoni.



Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments