Makubaliano ya amani sharti yaizuie Ukraine kujiunga na NATO - Urusi

Urusi itatafuta hakikisho kwamba Nato itaiondoa Ukraine kutoka kwa uanachama na kwamba Ukraine itasalia kutoegemea upande wowote katika makubaliano yoyote ya amani, naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema.
"Tutadai kuwepo kwa dhamana kubwa ya makubaliano haya," Alexander Grushko alikiambia chombo cha habari cha Urusi Izvestia.
"Sehemu ya dhamana hizi inapaswa kuwa hali ya kutoegemea upande wowote ya Ukraine mbali na kukataa kwa nchi za Nato kuikubali katika muungano," alisema.
Haya yanajiri huku Rais wa Marekani Donald Trump akisema kuwa atazungumza na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin siku ya Jumanne, huku mazungumzo yakiendelea kuhusu uwezekano wa kusitisha mapigano katika vita vya miaka mitatu nchini Ukraine.
Akizungumza kwenye Air Force One Jumapili jioni, Trump alisema: "Kazi nyingi zimefanywa mwishoni mwa juma. Tunataka kuona kama tunaweza kumaliza vita hivyo." "Tutakuwa tunazungumza kuhusu ardhi.
Tutazungumza kuhusu mitambo ya kuzalisha umeme," Trump alisema alipoulizwa kuhusu makubaliano.
Trump aliongeza kuwa tayari anajadili "kugawanya baadhi ya mali" kati ya Urusi na Ukraine.
Marekani na Ukraine zimekubaliana kupendekeza kusitisha mapigano kwa siku 30 kwa Urusi.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii



No comments