Mnyama anayetisha zaidi duniani' ashinda tuzo ya samaki bora wa mwaka New Zealand

Mara baada ya kutajwa kuwa mnyama anayetisha zaidi duniani kwa mwonekano wake , samaki aina ya blobfish amerejea kwa kishindo: ametangazwa wiki hii kama Samaki bora wa Mwaka na kikundi cha mazingira cha New Zealand.
Shindano hilo la kila mwaka, linalofanywa na Shirika la Mountain to Sea Conservation Trust, linalenga kuongeza ufahamu wa viumbe vya maji safi na viumbe vya baharini nchini New Zealand.
Mwaka huu, blobfish alishinda tuzo hiyo kwa karibu kura 1,300 kati ya zaidi ya kura 5,500 zilizopigwa. Samaki huyo aliye rojorojo huishi kando ya bahari na hukua na kufikia urefu wa nchi 12 (30cm).
Wao hupatikana hasa kwenye pwani ya Australia na Tasmania, ambapo wanaishi kwenye kina cha futi 2,000-4,000 (600-1,200m)chini ya bahari Ingawa blobfish hujulikana kwa umbo lake la kushangaza, kwa kweli hufanana na samaki wa kawaida.

Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii


No comments