Subscribe Us

Breaking News

PRINCE DUBE AMKIMBIZA ATEBA


MWAMBA Prince Dube mshambuliaji wa Yanga amemkimbiza kwenye suala la kucheka na nyavu mshambuliaji wa Simba, Leonel Ateba.

Wakali hawa wamekuwa na mwendelezo wao kwenye mechi ambazo wanacheza ndani ya uwanja huku Prince Dube akiwa nyota aliyeanza kwa kusuasua kabla ya gari kuwaka kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.

Ateba alianza kufunga kwenye mchezo dhidi ya Azam FC mzunguko wa kwanza wakiwa ugenini, kasi yake haijawa kwenye mwendelezo mzuri katika mechi za hivi karibuni akiwa na uzi wa Simba.

Dube anashikilia rekodi ya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga hat trick ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa na mpaka sasa ndani ya ligi ni mastaa watatu wamefunga hat trick ambapo wengine wawili waliofuata ni Aziz Ki wa Yanga na Steven Mukwala wa Simba.

Mabao 10 kibindoni anayo Dube akiwa mkali wakucheka na nyavu kutoka Yanga idadi ambayo ni sawa na mabao ya Clement Mzize ambaye naye ametupia mabao 10 kibindoni.

Mbali na kufunga mabao 10 Dube katengeneza pasi 7 za mabao akiwa ni miongoni mwa mastaa wenye pasi nyingi za mabao ambapo hapa kamkimbiza Ateba akiwa katoa pasi tatu za mabao.

Ateba ni mabao 8 kafunga ndani ya kikosi cha Simba kilichofunga jumla ya mabao 52 akihusika kwenye mabao 11 kwa kuwa katoa pasi tatu za mabao.

Kwenye mabao hayo 8 aliyofunga manne ni kwa pigo la penati huku Dube akiwa hajapewa jukumu la kupiga penati hivyo hajafunga bao la penati msimu wa 2024/25.



Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments