Subscribe Us

Breaking News

Televisheni ya Sudan yasema jeshi la nchi hiyo linakaribia kuchukua udhibiti wa Ikulu ya Rais kutoka kwa kundi la RSF


.

CHANZO CHA PICHA,AFP

Televisheni ya taifa ya Sudan imesema Alhamisi kwamba jeshi linakaribia kuchukua udhibiti wa Ikulu ya Rais huko Khartoum kutoka kwa Wanajeshi wa Rapid Support Forces RSF kuashiria mabadiliko makubwa katika mzozo wa miaka miwili ambao unatishia kuivunja nchi hiyo.

Siku ya Jumatano, mapigano makali yalizuka karibu na ikulu, huku milipuko ikisikika na mashambulizi ya anga ya jeshi yakilenga katikati mwa Khartoum, mashahidi na vyanzo vya kijeshi viliambia Reuters.

Baada ya takriban miaka miwili ya vita, RSF inadhibiti sehemu kubwa ya magharibi mwa Sudan na sehemu za mji mkuu wa Khartoum, lakini imekuwa ikipoteza nafasi katikati mwa Sudan kwa jeshi.

Makundi hayo mawili ya kijeshi yalifanya mapinduzi mwaka wa 2021, ambayo yalizuia mpito kwa utawala wa kiraia, na vita vilizuka mwezi Aprili 2023 baada ya mipango ya serikali mpya ya mpito kuzua mzozo mkali.

Vita hivyo vimesababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita mzozo mkubwa zaidi wa kibinadamu duniani, huku RSF na jeshi wakituhumiwa kwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.



Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments