Subscribe Us

Breaking News

Waasi wa M23 wawateka nyara wagonjwa 130 kutoka hospitalini - UN

c

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Maelezo ya picha,Waasi wa M23 wakiwa katika gari wakati wa kuwasindikiza waasi wa FDLR waliotekwa (hawapo pichani) kuelekea Rwanda kupitia kivuko cha mpaka wa Goma-Gisenyi Grande Barrier, Machi 1, 2025.

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wamefanya mashambulizi Mashariki mwa DR Congo na kuwateka nyara takribani wagonjwa na waliojeruhiwa 130 kutoka katika hospitali mbili za mji wa Goma wiki iliyopita, umesema Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu.

Wapiganaji wa M23 walivamia Hospitali ya CBCA Ndosho na Hospitali ya Heal Africa usiku wa Februari 28, na kuchukua wagonjwa 116 na 15, amesema msemaji wa Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Ravina Shamdasani.

Watu hao waliotekwa nyara wanashukiwa kuwa ni wanajeshi wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo au wanamgambo wanaoiunga mkono serikali wanaojulikana kwa jina la Wazalendo.

"Inasikitisha sana kwamba M23 inawanyakua wagonjwa katika vitanda vya hospitali kupitia uvamizi ulioratibiwa na kuwaweka katika maeneo yasiyojulikana," amesema Shamdasani, akitaka waachiliwe mara moja.

Wasemaji wa M23, Willy Ngoma na Lawrence Kanyuka Kingston hawakujibu maswali ya Reuters kuhusu tukio hilo.

Waasi wa M23 wanaoongozwa na Watutsi waliingia katika mji wa Goma mwishoni mwa Januari na tangu wakati huo wamepiga hatua kubwa kuelekea mashariki mwa Congo, wakiteka maeneo na kushikilia maeneo ya madini ya thamani.

Takriban watu 7,000 wameuawa mashariki mwa Congo tangu Januari na karibu watu nusu milioni wameachwa bila makazi baada ya kambi 90 za wakimbizi kuharibiwa katika mapigano hayo, kulingana na serikali.

No comments