Subscribe Us

Breaking News

India yapitisha muswada wenye utata kuhusu mali za Waislamu


dc

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Waislamu wameandamana kupinga mswada huo mpya

Baada ya saa kadhaa za mjadala mkali, bunge la India limepitisha muswada tata unaotaka kubadilisha usimamizi wa mali zenye thamani ya mabilioni ya dola zilizotolewa na Waislamu kwa karne nyingi.

Baraza la juu lilipitisha Muswada wa Marekebisho ya Waqf 2024, mapema siku ya Ijumaa, siku moja baada ya baraza la chini kuupitisha huku kukiwa na ukosoaji mkubwa.

Viongozi wa Kiislamu na vyama vya upinzani wanasema muswada huo "ni kinyume cha sheria" na unakiuka haki za jamii ya Waislamu walio wachache nchini India.

Lakini serikali inasema mswada huo unalenga kufanya usimamizi wa waqf (mali za Waislamu) kuwa wa wazi zaidi.

Muswada huo sasa utatumwa kwa rais wa India kupata idhini kabla ya kuwa sheria. Idhini hii inatarajiwa kuja hivi karibuni.

Waziri Mkuu Narendra Modi aliita kupitishwa kwa muswada huo ni “wakati wa mabadiliko,” kupitia chapisho kwenye X.

Ameandika, “mfumo wa waqf umekuwa na ukosefu wa uwazi na uwajibikaji kwa miongo kadhaa. Sheria iliyopitishwa na bunge itaongeza uwazi na pia kulinda haki za watu.”

Hata hivyo, upinzani umekuwa ukipinga mswada huo na kudai kuwa ni mbinu nyingine ya chama tawala cha Bharatiya Janata Party (BJP) kutatiza haki za walio wachache.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Congress Mallikarjun Kharge alibainisha kuwa wakati wanachama 288 walipiga kura ya kuunga mkono muswada huo katika bunge la chini, 232 waliupinga.

dfc

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,Asaduddin Owaisi, mbunge na rais wa chama cha All India Majlis-e-Ittehadul Muslimeen, ni mmoja wa wakosoaji wa muswada huo.

Tovuti ya sheria LiveLaw iliripoti Ijumaa kwamba mbunge Asaduddin Owaisi, rais wa chama cha All India Majlis-e-Ittehadul Muslimeen na mkosoaji mkali wa muswada huo, amepeleka kesi katika Mahakama ya Juu.

Waqfu ni mali inayotolewa sadaka au mchango wa kidini na Waislamu kwa manufaa ya jamii. Mali hii haiwezi kuuzwa au kutumika kwa madhumuni mengine yoyote.

Waqfu ni muhimu kwa Waislamu milioni 200 wa India kwani hutumiwa kwa misikiti, madrasa, makaburi na nyumba za watoto yatima.

Chini ya mswada mpya, bodi za Waqf lazima zitoe hati halali za kudai mali fulani kuwa ni waqfu. Na katika kesi ya migogoro - haswa juu ya ardhi - uamuzi wa mwisho utabaki kwa serikali.

Pili, mswada unapendekeza kuruhusu wasio Waislamu kuteuliwa kwenye bodi na mabaraza ya waqf.

Mswada huo pia unaruhusu uingiliaji wa mahakama katika mizozo - kuchukua nafasi ya mfumo wa awali ambapo maamuzi ya mabaraza ya waqf yalizingatiwa kuwa ya mwisho.

Mswada huo pia unapendekeza mfumo wa usajili, unaohitaji mali zote za waqf kusajiliwa ndani ya miezi sita kabla ya sheria kuanza kutekelezwa.

Maombi ya usajili mpya wa mali za waqf pia yanahitaji kuwasilishwa kwa bodi za waqfu kupitia mfumo huu.

Muswada huo pia una vifungu vinavyoipa serikali jukumu kubwa katika upimaji wa mali za waqf.


Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments