Subscribe Us

Breaking News

M23 waondoka katika mji wa Walikale kabla ya mazungumzo ya Qatar


ERF

CHANZO CHA PICHA,ALE

Maelezo ya picha,Waasi wa M23

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wamejiondoa katika mji wa kimkakati wa Walikale, wakielezea hatua hiyo kama ishara ya nia njema kabla ya mazungumzo ya amani na serikali wiki ijayo.

M23 imeteka miji miwili mikubwa mashariki mwa Congo tangu Januari ambayo yamesababisha maelfu ya vifo na mamia kwa maelfu kuhama makazi yao.

Mapigano hayo yamezusha hofu ya kutokea vita vya kikanda, huku majirani wa Congo, Uganda na Burundi pia wakiwa na wanajeshi katika eneo hilo. Serikali ya Congo na M23 wanapanga kufanya mazungumzo yao ya kwanza ya moja kwa moja huko Doha wiki hii.

Walikale uko kando ya barabara inayounganisha mikoa minne ya mashariki mwa Congo, iko katika eneo lenye madini mengi yakiwemo ya bati.

M23 iliahidi kujiondoa Walikale mwezi uliopita lakini ilishindwa kufanya hivyo, ikilishutumu jeshi la Congo kutotimiza ahadi zake na kuondoa ndege zisizo na rubani.

Wakazi wawili na afisa wa eneo hilo walithibitisha kwa Reuters wiki hii kwamba M23 wameondoka katika mji huo. Msemaji wa jeshi Sylvain Ekenge aliambia Reuters siku ya Ijumaa wanajeshi wa Kongo wako huko, na kuthibitisha M23 wameondoka.



Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments