SIMBA WANASA SIRI ZA WAARABU, KAZI KUBWA KUFANYIKA
KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema kuwa wamepata muda wa kuwafutilia wapinzani wao Al Masry na kutambua kuwa ni miongoni mwa timu ambayo ina nguvu ubwa kwenye ulinzi na kushambulia jambo ambalo watakabiliana nalo ili kupata matokeo chanya.
Kikosi cha Simba kipo nchini Misri kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ambao ni hatua ya robo fainali unatarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025, robo fainali ya pili inatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 9 2025.
Ikumbukwe kwamba Machi 28 kikosi cha Simba kilikwea pipa kutoka Tanzania mpaka Cairo kisha wakaelekea kuweka kambi katika mji wa Ismailia ambapo waliweka kambi na wachezaji waliokuwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania ikiwa ni Mohamed Hussen, Kibu Dennis, Shomari Kapombe nao wapo kambini.
Fadlu amesema: “Tunaendelea na maandalizi wachezaji wanajitahidi kuendana na mazingira ya hali ya hewa ambayo yapo kwa sasa na tupo tayari kwa kuwa wachezaji wapo tayari kuelekea mchezo wetu na hakuna presha ambayo ipo kuelekea kwenye mchezo wetu.
“Ukiangalia rekodi tumekuwa na matokeo kwenye mechi za kimataifa kwa mechi ambazo tulicheza ugenini hivyo hilo halitupi presha kuelekea kwenye mchezo wetu. Al Masry ni miongoni mwa timu ambazo zina muungano mzuri.
“Ukitazama namna ilivyo imara kwenye ulinzi, ushambuliaji inakuja na mitindo tofautitifauti kwenye mechi ambazo wanacheza lakini kwa yote hayo tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo wetu. Mechi haitakuwa nyepesi na kikubwa ambacho tunahitaji ni kuona kwamba tunapata mabao kwenye mchezo wetu.”
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii




No comments