SIMBA SC KUACHANA NA KIPA HUYU MAZIMA
INAELEZWA kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa msimu wa 2025/26 kipa wa Simba SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Ayoub Lakred asiwe ndani ya kikosi hicho.
Habari zinasema kuwa kipa wa Simba, Ayoub Lakred kwa sasa kuna timu mpya ambayo ameipata na ataitumikia kwa msimu ujao kuendelea na majukumu yake.
Ni dili la miaka miwili amepata kwenye timu hiyo mpya. Simba SC ipo tayari kumuachia kwa sasa kwa kuwa hajawa chaguo la kwanza la kocha kutokana na kutokuwa fiti kwa muda mrefu.
Msimu wa 2024/25 wakati Simba SC kwa mara nyingine ikipishana na mataji yote, kipa huyo hakuwa chaguo la kwanza mbele ya Fadlu.
Katika mechi 30 za ligi hakupata nafasi ya kuanza mchezo hata mmoja zaidi alikuwa akiishia kwenye mazoezi Bunju na KMC Complex.
Ikumbukwe kwamba wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa 2024/25 Simba SC walieleza kuwa kipa huyo alipata maumivu kwenye maandalizi ya msimu mpya kambini Misri.
Moussa Camara alikuwa kipa namba moja kwa msimu wa 2024/25. Mechi ambazo alikaa langoni ni 28 kati ya 30 na alikusanya hati safi 19 akifungwa mabao 13.
Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa
app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii




No comments