Jonathan Ikangalombo kukiwasha rasmi Yanga

Yanga itakuwa wageni wa Mashujaa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, mjini Kigoma na Kocha Miloud Hamdi ameondoka na winga Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’ aliyesajiliwa dirisha dogo kwa ajili ya mchezo huo, huku akiweka wazi jamaa yupo tayari kukiwasha kwani kila kitu kwake sasa kipo freshi.
.
Akizungumza, Hamdi alisema Ikanga ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na anataka kuanza kumpa muda wa kucheza, kwani anamwona yuko sawa na hana uzito kama awali.
.
“Kuhusu ishu ya uzito wa mwili niliikuta hiyo taarifa, lakini kwa sasa sioni kisingizio hicho tena na ameonyesha kitu kikubwa mazoezini,” alisema Hamdi na kuongeza; “Ikanga ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na ninataka kuanza kumpa muda wa kucheza, nimemuangalia kwa kipindi hiki kifupi namuona ni winga mzuri akipewa nafasi.”
No comments