Subscribe Us

Breaking News

Vikosi vya usalama vya Syria vinatuhumiwa kuwanyonga makumi ya Waalawi


g

CHANZO CHA PICHA,REUTERS

Vikosi vya usalama vya Syria vinadaiwa kuwaua makumi ya watu wa jamii ya wachache ya Alawite katika mkoa wa pwani wa Latakia, kulingana na kundi la ufuatiliaji wa vita.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria lenye makao yake makuu nchini Uingereza (SOHR) lilisema kuwa raia 162 wameuawa katika "unyongaji uwanjani" katika eneo hilo - kitovu cha rais aliyeondolewa madarakani Bashir al-Assad, ambaye pia ni mfuasi wa dhehebu la Waalawi.

Chanzo cha wizara ya mambo ya ndani kililiambia shirika rasmi la habari la nchi hiyo Sana kwamba "ukiukwaji wa haki za watu binafsi" ulifanyika kwenye pwani na kuahidi kukomesha.

Habari za BBC hazijaweza kuthibitisha madai kwamba mauaji hayo yalifanywa na vikosi vya watawala wapya wa Syria.




Download/Pakua/Install App ya Abedijr kupitia google crome Bofya Hapa

                               app hii aipatikani google playstore ka sasa hupatikana kwenye wavuti yetu hii 

No comments